Naibu Katibu Idara ya Ajira katika Sekretarieti ya Ajira, Bw. Lucas Mrumapili akichangia mada katika kikao cha Baraza kilichofanyika SUA mkoani Morogoro.
Jan 25, 2021
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mipango, Tathmini na Ufuatiliaji katika Sekretarieti ya Ajira, Bw. Godfrey Mchani akiwasilisha mada ya masuala ya bajeti katika kikao cha Baraza kilichofanyika SUA mkoani Morogoro.
Jan 25, 2021
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi katika Sekretarieti ya Ajira wakiwa katika kikao cha Baraza kilichofanyika SUA mkoani Morogoro.
Jan 25, 2021
Baadhi ya Watumishi wa Sekretarieti ya Ajira wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi lililofanyika SUA mkoani Morogoro.
Jan 25, 2021
Katibu Muhutasi Mwandamizi, Bi. Janeth Saki akichapa majadiliano mbalimbali ya Wajumbe wakati wa kikao cha Baraza kilichofanyika SUA mkoani Mororogoro.
Jan 25, 2021
mmoja wa wasimamizi wa usaili ambae ni Naibu Katibu Idara ya Udhibiti wa Ubora, Bw. Humphrey Mniachi akiangalia wasailiwa kama wanafuata taratibu za usaili wakati wasailiwa hao wakiendelea na usaili wa kuandika mkoani Dodoma.
Jan 25, 2021
Wasailiwa wa nafasi mbalimbali za kazi kwa ajili ya MORUWASA wakiendelea na usaili SUA mkoani Morogoro.
Jan 25, 2021
Baadhi ya Wasimamizi na Walimu wakipokea maelekezo kutoka kwa mratibu wa zoezi hilo Bw. Ally Mnyimwa jijini Dodoma.
Jan 25, 2021
Baadhi ya Wasailiwa wakiendelea na usaili wa kuandika jijini Dodoma.
Dec 21, 2020
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Kapt. Mstaafu George Mkuchika akiwasili katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine Mkoani Morogoro kwa ajili ya kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Ajira kushoto kwake ni Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi
Dec 19, 2020
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Kapt. Mstaafu George Mkuchika akisalimiana na Katibu wa TUGHE wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Issa Paul alipowasili katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine kwa ajili ya kufungua kikao cha Baraza la Sekretarieti ya Ajira.
Dec 19, 2020
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Kapt. Mstaafu George Mkuchika akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro.
Dec 19, 2020
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi akiwa katika kikao cha Wakaguzi wa Nje pamoja na Wajumbe wa Menejimenti wa Taasisi yake.
Dec 19, 2020
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Kapt. Mstaafu George Mkuchika akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali mara baada ya kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kilichofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro.
Dec 19, 2020
Wakaguzi wa Nje wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, wakiongozwa na Mkaguzi Mkuu Bw. Emmanuel Shirima kulia ni Bw. Erasto Kawili na Bw. Semboko kwenye kikao na Menejimenti ya Sekretarieti ya Ajira hawapo pichani.
Dec 19, 2020
Mhasibu Mkuu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Sulemani Mwanga akiwa na Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani Bw. John Kiria wakisikiliza hoja kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Nje Bw. Emmanuel Shirima.
Dec 19, 2020
Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakifuatilia kikao cha Wakaguzi wa Nje hawapo pichani.
Dec 19, 2020
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Xavier Daudi akiongea na Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda alipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Sekretarieti ya Ajira lililofanyika chuoni hapo.
Dec 19, 2020
Baadhi ya Watumishi wa Sekretarieti ya Ajira wakimsikiliza Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi katika kikao chao cha kwanza tangu wahamie Dodoma.
Dec 19, 2020
Naibu Katibu, Idara ya Ajira, Bw. Lucas Mrumapili akiwa na Naibu Katibu, Idara ya Udhibiti wa Ubora, Bw. Humphrey Mniachi wakimsikiliza Katibu wa Sekretarieti ya Ajirakatika Utumishi wa Umma hayupo picha Bw. Xavier Daudi ikiwa ni kikao cha kwanza tangu ofisi za Sekretarieti ya Ajira zihamie Dodoma.
Dec 19, 2020
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi katikati akitoka kukagua ofisi za Watumishi wa Idara ya Ajira na kulia ni Naibu Katibu, Idara ya Ajira Bw. Lucas Mrumapili na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Bw. Innocent Bomani.
Dec 06, 2020
Katibu, Menejimenti na Watumishi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wanakupongeza kwa kuteuliwa kwa mara nyingine kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Huruma Mkuchika (Mb).
Dec 06, 2020
Katibu, Menejimenti na Watumishi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wanakupongeza kwa kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius John Ndejebi (Mb).
Nov 26, 2020
Wajumbe wa jopo la usaili ambao miongoni mwao kuna Makatibu Wakuu Wastaafu na Viongozi wengine Waandamizi Serikalini wakimsikiliza mmoja wa wasailiwa ngazi ya Menejimenti TASAF akiwa nchini Botswana hayupo pichani akifanya usaili kwa njia ya mtandao (Video Conference).
Nov 26, 2020
Katikati ni Katibu Mkuu Utumishi-Dkt. Laurean Ndumbaro akijadiliana jambo na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi na kushoto kwake ni Katibu Mkuu, IKULU- Dkt. Moses Kusiluka wakati wa usaili wa nafasi ya menejimenti TASAF, mmoja wa wasailiwa akiwa nchini Botswana. Usaili umefanyika TAGLA kwa njia ya mtandao (Video Conference).
Nov 26, 2020
Katibu Mkuu Utumishi-Dkt. Laurean Ndumbaro akiongoza jopo la usaili wa nafasi ya Menejimenti TASAF, kushoto kwake ni Katibu Mkuu Ikulu- Dkt. Moses Kusiluka, kulia kwake ni Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi, Mtendaji Mkuu wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga pamoja na Katibu Mkuu Mstaafu Dkt. Silvanus Likwelile wakimsikiliza mmoja wa wasailiwa akiwa nchini Botswana wakati wa usaili kwa njia ya mtandao (Video Conference).
Nov 26, 2020
Moja ya gari la jeshi likifungwa mlango tayari kuondoka mara baada ya kushusha mizigo kwenye ofisi za Sekretarieti ya Ajira jijini Dodoma.
Nov 26, 2020
Moja ya gari la jeshi likiwa limewasili katika jengo la Utumishi zilipo pia ofisi za Sekretarieti ya Ajira jijini Dodoma tayari kushusha mizigo ya ofisi hiyo.
Nov 26, 2020
Mizigo ya Sekretarieti ya Ajira ikiendelea kushushwa kwenye gari la jeshi jijini Dodoma ilipohamia taasis hiyo.
Nov 26, 2020
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Xavier Daudi akiwa na watumishi wengine wakiangalia moja ya gari likiondoka na mizigo katika ofisi hizo eneo la Kivukoni jijini Dar es Salaam na gari lingine likiwa tayari kuanza safari kuelekea jijini Dodoma walipohamia.
Nov 26, 2020
Wasailiwa wakifanya na Usaili wa Mchujo wa nafasi za kazi za Taasisi mbalimbali za Umma, jijini Mwanza .
Nov 26, 2020
Mmoja wa madereva wa gari la Jeshi la Wananchi lililopakia mizigo ya Sekretarieti ya Ajira, Staff Surgent Aisha Kigodi akielekea kwenye gari eneo la Kivukoni jijini Dar es Salaam tayari kuanza safari kuelekea jijini Dodoma zilipohamia ofisi za taasis hiyo.
Nov 26, 2020
Haya ni baadhi ya magari ambayo yamekuwa yakitumika kwenye Usaili wa Vitendo kwa ajili ya madereva wenye leseni kuanzia daraja C1 au daraja E.
Nov 11, 2020
Menejimenti na Watumishi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wanampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchaguliwa kwao kwa kishindo kuiongoza Tanzania kwa awamu nyingine ya miaka mitano.
Nov 11, 2020
Menejimenti na Watumishi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wanampongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo.
Oct 09, 2020
Menejimenti na Watumishi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wanampongeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kwa kuaminiwa na kuteuliwa kwake kwa mara nyingine kuwatumikia Watanzania,
Oct 09, 2020
Naibu Katibu, Idara ya Ajira katika Sekretarieti ya Ajira Bw. Lucas Mrumapili akinukuu baadhi ya hoja wakati wa kikao cha Wafanyakazi wakizungumza na Mkuu wa taasisi na wengine ni Maafisa wa Sekretarieti ya Ajira wakifuatilia hoja mbalimbali.
Oct 09, 2020
Baadhi ya Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Katibu wa taasisi hiyo, Bw. Xavier Daudi hayupo pichani wakati wa kikao cha pamoja na Wafanyakazi hao.
Oct 09, 2020
Mhe. Balozi Anisa Mbega aliyesimama mbele katikati akiwa na baadhi wa Maafisa Waandamizi kutoka Sekretarieti ya Ajira na wadau wengine wa sekta ya Ajira serikalini wakati wa kikao cha pamoja cha wadau kujadili mahitaji ya kipaumbele ya Serikali kutoka kwa Watanzania wataalam wenye ujuzi maalum waliopo nje ya nchi (Diaspora) kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 6, 2020.
Oct 09, 2020
Mhe. Balozi Anisa Mbega aliyeketi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa na baadhi wa Maafisa Waandamizi kutoka Sekretarieti ya Ajira na wadau wengine wa sekta ya Ajira serikalini wakati wa kikao cha pamoja cha wadau kujadili mahitaji ya kipaumbele ya Serikali kutoka kwa Watanzania wataalam wenye ujuzi maalum waliopo nje ya nchi (Diaspora) kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 6, 2020.
Sep 28, 2020
Naibu Katibu, Idara ya Ajira katika Sekretarieti ya Ajira Bw. Lucas Mrumapili akizungumza na Wajumbe wa Majopo ya Usaili katika Chuo cha CBE jijini Mwanza kabla ya kuanza usaili wa wa kujaza nafasi za kazi za Mkataba TANESCO.
Sep 28, 2020
Baadhi ya Wasailiwa wa nafasi mbalimbali za kazi za TANESCO wakiendelea na Usaili wa Mchujo jijini Mwanza katika Chuo cha Ualimu Butimba.
Sep 28, 2020
Baadhi ya Wasailiwa wa nafasi mbalimbali za kazi za TANESCO wakiendelea na Usaili wa Mchujo jijini Mwanza katika Chuo cha Ualimu Butimba.
Sep 28, 2020
Baadhi ya Wasailiwa wa nafasi mbalimbali za kazi za TANESCO wakiendelea na Usaili wa Mchujo jijini Mwanza katika Chuo cha Ualimu Butimba.
Sep 03, 2020
Mtaalam wa masuala ya Saikolojia, Zainab Rashid kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii akifundisha washiriki wa mafunzo kutoka Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma namna ya kuweza kumpima mtu na kuweza kufahamu tabia, uwezo na hulka ya mhusika.
Sep 03, 2020
Wataalam wa Saikolojia kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii kulia ni Gilbert Mkisi, Zainab Rashid na Julius Mbilinyi wakinukuu maswali ya kutoka kwa Washiriki ili kuweza kuyapatia majibu.
Sep 03, 2020
Washiriki wa Mafunzo ya Saikolojia kutoka Sekretarieti ya Ajira pamoja na Wawezeshaji masuala ya Saikolojia kutoka katika Vyuo mbalimbali nchini wakiwa katika picha ya pamoja.
Sep 03, 2020
Mtaalam wa masula ya Saikolojia Justine Kavindi kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akifafanua jambo kwa Washiriki wa mafunzo kutoka Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Sep 03, 2020
Wataalam wa Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma Dkt. Pambas Basil, na Dkt. Florentina Nsolenzi na mwingine ni Afisa Utumishi Mkuu katika Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bi. Consolatha Bura.
Sep 03, 2020
Dkt. Bertha Losioki, kulia kwake ni Miraji Mgonja na mwingine ni Justine Kavindi ambao ni wataalam wa masuala ya Saikolojia katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere walipokuwa wakitoa mafunzo kwa Washiriki wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Aug 27, 2020
Kulia ni SP Deus Sokoni akizungumza wakati kikao kazi baina ya Watendaji wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Jeshi la Polisi nchini- Usalama Barabarani Makao Makuu pamoja na wadau kutoka Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na kushoto kwake ni ASP Ibrahim Samwix akinukuu baadhi ya mambo waliyokubaliana.
Aug 27, 2020
Kushoto ni SP Deus Sokoni akiwa Maafisa wengine kutoka Jeshi la Polisi nchini wakinukuu baadhi ya mambo waliyokubaliana wakati kikao kazi baina ya Watendaji wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Jeshi la Polisi nchini- Usalama Barabarani Makao Makuu na wadau kutoka Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Aug 27, 2020
Naibu Katibu, Idara ya Udhibiti wa Ubora katika Sekretarieti ya Ajira, Bw. Humphrey Mniachi akiongea na baadhi ya wadau kutoka Jeshi la Polisi nchini- Usalama Barabarani Makao Makuu na Chuo cha Mafunzo Ufundi Stadi (VETA) hawapo pichani kulia kwake ni Afisa Rasilimaliwatu Bw. Ally Mnyimwa.
Aug 27, 2020
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Bi. Clara Kibodya akinukuu baadhi ya mambo waliyojadiliana katika kikao kazi baina ya Watendaji kutoka Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Jeshi la Polisi nchini- Usalama Barabarani Makao Makuu na VETA.
Aug 27, 2020
Mkufunzi Mkuu wa masuala ya ufundi na Udereva kutoka Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Bw. Kisembe Kapele akifafanua jambo wakati wa kikao kazi kilichohusisha wataalamu kutoka Jeshi la Polisi nchini-Usalama Barabarani Makao Makuu, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma pamoja na Wataalam wengine kutoka VETA.
Aug 19, 2020
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo katika Sekretarieti ya Ajira wakibadilishana mawazo baada ya kikao, kulia ni Bw. Humphrey Mniachi, Bw. Lucas Mrumapili, Mhandisi Samwel Tanguye na Bi. Toni Mbilinyi.
Aug 19, 2020
Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi Bi Nester Mbilinyi akitoa mafunzo ya mfumo wa TANePS kwa Wajumbe wa Menejimenti ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Aug 19, 2020
Baadhi ya Maafisa Waandamizi katika Sekretarieti ya Ajira, kushoto ni Bw. Humphrey Mniachi, Mhandisi Samwel Tanguye na Bw. Innocent Bomani wakimsikiliza Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mipango hayuko pichani Bw. Godfrey Mchani.
Aug 14, 2020
Baadhi ya Wahitimu wa Ufundi Seremala wakiwa katika usaili wa vitendo VETA jijini Dar es Salaam.
Aug 14, 2020
Mmoja wa vijana wa ufundi VETA akifungua ili kukirekebisha kifaa cha gari wakati wa usaili wa vitendo.
Aug 07, 2020
Naibu Katibu, Idara ya Ajira katika Sekretarieti ya Ajira Bw. Lucas Mrumapili akitoa maelekezo ya jumla kwa Wasailiwa wakati wa usaili wa mchujo uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Aug 07, 2020
Naibu Katibu, Idara ya Udhibiti wa Ubora katika Sekretarieti ya Ajira Bw. Humphrey Mniachi akipitia namba za Wasailiwa kabla ya kuzituma katika akaunti zao kwenye mfumo wa maombi ya kazi.
Jul 06, 2020
Mmoja wa Wasimamizi wa Usaili akiangalia Wasailiwa wakiendelea na Usaili (DUCE) kwa ajili ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT).
Jul 06, 2020
Mabegi ya Wasailiwa yakiwa mbele wenyewe wakiendelea na Usaili (DUCE) kwa ajili ya nafasi za kazi za Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT).
Jul 06, 2020
Baadhi ya Wasailiwa wa nafasi za kazi kwa ajili ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) wakiendelea na Usaili (DUCE).
Jun 01, 2020
Katibu Mkuu, (OR-MUUB), Dkt. Laurian Ndumbaro akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira, Mazizini-Zanzibar.
Jun 01, 2020
Katibu Mkuu, (OR-MUUB), Dkt. Laurian Ndumbaro akiingia katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira eneo la Mazizini-Zanzibar, nyuma yake ni Katibu wa Ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi na Mkurugenzi wa Mipango na Rasilimaliwatu (OR-UUUB) Bw Khamis Juma.
Jun 01, 2020
Baadhi ya Watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, wakiwa nje ya ofisi hiyo eneo la Mazizini-Zanzibar.
Jun 01, 2020
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango ya Rasilimaliwatu (OR-UUUB- Zanzibar Bw. Khamis Juma akitoa ufafanuzi kwa Makatibu Wakuu wakati wa makabidhiano ya ofisi za Sekretarieti ya Ajira, Mazizini- Zanzibar.
Jun 01, 2020
Katibu Mkuu, (OR-MUUB), Dkt. Laurian Ndumbaro akiongea wakati wa makabidhiano ya ofisi za Sekretarieti ya Ajira Mazizini- Zanzibar, kushoto ni Katibu Mkuu, (OR-UUUB), Bw. Yakout Hassan Yakout na Naibu Katibu (OR-UUUB).
Jun 01, 2020
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi akiwasilisha taarifa yake wakati wa makabidhiano ya ofisi za Sekretarieti ya Ajira, Mazizini- Zanzibar
Jun 01, 2020
Katibu Mkuu, (OR-MUUB), Dkt. Laurian Ndumbaro akiwa Katibu Mkuu, (OR-UUUB), Bw. Yakout Hassan Yakout pamoja na Viongozi na Watendaji wengine wakati wa makabidhiano ya ofisi za Sekretarieti ya Ajira, Mazizini-Zanzibar
Jun 01, 2020
Katibu Mkuu, (OR-UUUB), Bw. Yakout Hassan Yakout akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira, Mazizini-Zanzibar
May 22, 2020
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi akitoa maelekezo kwa Wasimamizi wa Usaili (hawapo pichani) kuhusu masuala ya kuzingatia wakati wa usimamizi wa usaili mwingine ni Katibu Msaidizi Idara ya Ajira Bi. Khadija Isihaka.
May 22, 2020
Naibu Katibu Idara ya Udhibiti na Ubora katika Sekretarieti ya Ajira Bw. Humphrey Mniachi akitoa ufafanuzi kwa Wasimamizi wa Usaili (hawapo pichani) kuhusu usimamizi wa usaili mwingine ni Katibu Msaidizi Idara ya Ajira Bi. Khadija Isihaka.
May 22, 2020
Wasailiwa wakiendelea na usaili wa kuandika kwa ajili ya kujaza nafasi mbalimbali za kazi zilizotangazwa na Kibaha Education Centre kupitia Sekretarieti ya Ajira.
May 22, 2020
Baadhi ya Wasailiwa wakiendelea na usaili wa kuandika kwa ajili ya kujaza nafasi mbalimbali za kazi zilizotangazwa na Kibaha Education Centre kupitia Sekretarieti ya Ajira.
May 22, 2020
Maafisa Tawala wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kushoto ni Bw. Issa Paul na Bw. Mwita Werema wakiandaa rasimu ya tangazo la nafasi wazi za kazi.
May 22, 2020
Afisa Utumishi Mwandamizi katika Sekretarieti ya Ajira Bi. Judith Usangira akipata ufafanuzi wa masuala ya Watumishi kutoka kwa Afisa Utumishi Bw. Imani Kasagara.
May 22, 2020
Afisa Rasilimaliwatu Mkuu Bw. Innocent Bomani wa Sekretarieti ya Ajira akipitia nyaraka aliyopelekewa na Dereva Mwandamizi Bw. Christopher Ngazi aliyesimama kabla ya kuipitisha.
May 22, 2020
Watumishi wa Idara ya Utawala katika Sekretarieti ya Ajira wakipitia moja orodha ya vifaa vinavyohitajika kununuliwa kulia ni Bi. Neema Kivugo, Bw. Malatika Mbaga na Mlagwa Nyasebwa.
May 05, 2020
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi akiongoza jopo la usaili wa nafasi ya kazi ngazi ya Menejimenti kwa ajili ya UCSAF ambao umefanyika TAGLA jijini Dar es Salaam kwa njia ya "Video Conference".
May 05, 2020
Mmoja wa Wasailiwa wa nafasi ya kazi ngazi ya Menejimenti kwa ajili ya UCSAF akifanya usaili kwa njia ya "Video Conference" ambao umefanyika katika ofisi za TAGLA jijini Dar es Salaam.
May 05, 2020
Wajumbe wa jopo la usaili wa UCSAF wakimsikiliza mmoja wa Wasailiwa wa nafasi ya kazi ya Menejimenti hayupo pichani, ambapo usaili huo umefanyika katika ofisi za TAGLA kwa njia ya ''video conference''
Apr 16, 2020
Mwenyekiti wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bi Rose Lugembe akisisitiza jambo kwa Wajumbe katika moja ya vikao vya bodi hiyo.
Apr 16, 2020
Katibu wa wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi akiongea katika moja ya vikao vya Menejimenti na kushoto kwake ni Afisa Utumishi Mkuu katika ofisi hiyo Bw. Innocent Bomani akinukuu dondoo za kikao.
Apr 16, 2020
Katibu Msaidizi (Idara ya Ajira), Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Malimi Muya akiongea na Waandishi wa Habari, hawapo pichani kuhusu uendeshaji wa mchakato wa ajira serikalini.
Mar 10, 2020
Tuwaenzi mama zetu, dada zetu, hawa ni baadhi ya Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Ajira wakiwa katika viwanja vya Leaders katika Siku ya Maadhimisho ya Wanawake Duniani.
Mar 10, 2020
Tuwaenzi mama zetu, dada zetu, hawa ni baadhi ya Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Ajira wakiwa katika viwanja vya Leaders katika Siku ya Maadhimisho ya Wanawake Duniani.
Mar 10, 2020
Tuwaenzi Mama zetu na Dada zetu, pichani ni baadhi ya Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Ajira wakiwa katika Viwanja vya Leaders katika Siku ya Maadhimisho ya Wanawake Duniani.
Mar 05, 2020
Katibu Msaidizi, Idara ya Ajira katika Sekretarieti ya Ajira Bw. Malimi Muya akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari hawapo pichani waliotaka kufahamu maboresho yaliyofanyika katika uendeshaji wa mchakato wa ajira.
Mar 05, 2020
Naibu Katibu Idara ya Ajira katika Sekretarieti ya Ajira Bw. Lucas Mrumapili akiwasilisha taarifa ya usaili uliopita mbele ya Wajumbe hawako pichani, kushoto ni Katibu Msaidizi Bi Khadija Isihaka na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bi. Victoria Fovo.
Feb 21, 2020
Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi katika Sekretarieti ya Ajira Bw. Robert Makenge akiwasilisha mada ya namna bora ya kuagiza mahitaji ya ofisi kwa mujibu wa taratibu za Ununuzi wa Umma kwa Watumishi wa ofisi hiyo.
Jan 09, 2020
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi akielekeza jambo kwa Maafisa Waandamizi wa taasisi hiyo waliosisimama ambao ni Bw. Godfrey Mchani na Bw. Dunia Kanena.
Jan 09, 2020
Baadhi ya Maafisa Waandamizi katika Sekretarieti ya Ajira wakipitia taarifa ya Tathmini na Ufuatiliaji kabla ya kuiwasilisha kwenye kikao cha Menejimenti, kulia ni Bw. Dunia Kanena, Mussa Mselem na Godfrey Mchani.
Jan 09, 2020
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi akiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Bi Victoria Fovo wakipitia moja ya nyaraka kabla ya kuanza kwa kikao cha Menejimenti.
Jan 02, 2020
Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Ajira Bi Rose Lugembe akiteta jambo na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi wakati wa kikao kazi.
Jan 02, 2020
Baadhi ya Watendaji wa Sekretarieti ya Ajira wakiwa katika kikao cha Wajumbe wa Sekretarieti hio wakati wa kupitia matokeo ya usaili, kulia ni Bi Victoria Fovo, Bw. Lucas Mrumapili, Bi. Khadija Isihaka na Bw. Malatika Mbaga
Jan 02, 2020
Baadhi ya Watumishi wa Sekretarieti ya Ajira wakifuatilia mada ya namna bora ya matumizi ya vifaa vya TEHAMA wakati wa semina ya mafunzo kazini iliyokuwa ikitolewa na Afisa Tehama wa Taasisi hiyo Bw. Hemed Mkomwa hayupo pichani.
Jan 02, 2020
Baadhi ya Watumishi wa Sekretarieti ya Ajira wakimsikiliza Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi katika semina iliyoandaliwa na ofisi hiyo kwa lengo la kujengeana uwezo ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa.
Jan 02, 2020
Katibu wa Mfuko wa kusaidiana (MKUSA) wa wanachama wa Sekretarieti ya Ajira, Mhandisi Samweli Tanguye akisoma ripoti ya mwaka kwa Wanachama wa mfuko huo (hawapo pichani) kulia kwake ni Mwenyekiti wa Mfuko Bi. Riziki Abraham.
Jan 02, 2020
Katibu wa Mfuko wa kusaidiana (MKUSA) wa wanachama wa Sekretarieti ya Ajira, Mhandisi Samweli Tanguye akisoma ripoti ya mwaka kwa Wanachama wa mfuko huo (hawapo pichani) kulia kwake ni Mwenyekiti wa Mfuko Bi. Riziki Abraham.
Jan 02, 2020
Baadhi ya Watumishi wa Sekretarieti ya Ajira wakimsikiliza Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi katika semina iliyoandaliwa na ofisi hiyo kwa lengo la kujengeana uwezo ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa.
Jan 02, 2020
Baadhi ya Watumishi wa Sekretarieti ya Ajira wakifuatilia mada ya namna bora ya matumizi ya vifaa vya TEHAMA wakati wa semina ya mafunzo kazini iliyokuwa ikitolewa na Afisa Tehama wa Taasisi hiyo Bw. Hemed Mkomwa hayupo pichani.
Jan 02, 2020
Baadhi ya Watendaji wa Sekretarieti ya Ajira wakiwa katika kikao cha Wajumbe wa Sekretarieti hio wakati wa kupitia matokeo ya usaili, kulia ni Bi Victoria Fovo, Bw. Lucas Mrumapili, Bi. Khadija Isihaka na Bw. Malatika Mbaga
Jan 02, 2020
Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Ajira Bi Rose Lugembe akiteta jambo na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi wakati wa kikao kazi.
Nov 18, 2019
Naibu Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Idara ya TEHAMA, Mhandisi Samweli Tanguye akitoa mafunzo ya Mfumo wa Ajira kwa baadhi ya Waajiri wa Sekta ya Umma.
Nov 18, 2019
Mwenyekiti wa Chama cha Shule Binafsi za Udereva Tanzania (CHASHUBATA) Bw. Jonas Bigaye akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na watendaji wa Sekretarieti ya Ajira kilichofanyika katika katika ukumbi wa Sekretarieti ya Ajira kilicholenga kujadili namna ya kuboresha mafunzo yanayotolewa na vyuo hivyo.
Nov 18, 2019
Katibu Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi (aliyesimama) akifafanua jambo kwa ugeni kutoka Tume ya Utumishi wa Umma nchini Zimbabwe walipotembelea Ofisi za Sekretarieti ya Ajira.
Nov 18, 2019
Mhandisi Samweli Tanguye ambaye ni Naibu Katibu (TEHAMA) ,akitoa mada ya mabadiliko ya Mfumo wa uombaji kazi kwa wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma chini Zimbabwe walipofanya ziara ya mafunzo nchini.
Nov 18, 2019
Wajumbe wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma katika moja ya kikao wakipitia majina ya waombaji Ajira Serikalini.
Nov 06, 2019
Naibu Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Idara ya Udhibiti na Ubora Bw. Humphrey Mniachi akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali katika Chama cha Shule Binafsi za Udereva Tanzania (CHASHUBUTA), kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Sekretarieti ya Ajira. Kushoto ni Bw. Ally Mnyimwa.
Aug 11, 2019
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Anold Kihaule (kulia na kushoto kwake) ni Naibu Katibu Idara ya TEHAMA katika Sekretarieti ya Ajira Mhandisi Samwel Tanguye.