UFAFANUZI WA TANGAZO LA KUITWA KAZINI LA TAREHE 25 JANUARI, 2021

Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuomba radhi kwa makosa yaliyofanyika katika tangazo la kuitwa kazini lililotoka tarehe 25 Januari, 2021 lenye Kumb. Na. EA.7/96/01/L/22 la MDA’s na LGA’s kuwa baadhi ya majina ya wasailiwa na sehemu waliko pangiwa kituo cha kazi zilitolewa kimakosa.

 

Hivyo, Watumishi walioonekana kuitwa kazini kwa mara ya pili katika ofisi hizo hizo ilihali wamekwisha ripoti katika taasisi zifuatazo:- Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC), Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (IAE), Hospitali ya Kikristo Kilimanjaro (KCMC), na Halmashauri ya Wilaya ya Katavi, tunaomba waendelee na majukumu yao kama kawaida katika ofisi husika.

 

Aidha, ofisi ambazo Wasailiwa wake wameitwa kazini hivi sasa ni hizi zifuatazo:-

  1. Wizara ya Mifugo na Uvuvi,
  2. Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea,
  3. Halmashauri ya Wilaya ya Igunga,
  4. Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga,
  5. Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua,
  6. Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo,
  7. Halmashauri ya Wilaya ya Manspaa ya Musoma,
  8. Halmashauri ya Wilaya ya Njombe,
  9. Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba,
  10. Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),
  11. Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI),
  12. Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE),
  13. Chuo Kikuu Mzumbe – MU,
  14. Chuo Kikuu cha Dodoma – UDOM,
  15. Chuo Kikuu Ardhi – ARU,
  16. Chuo cha Taifa cha Usafirishaji – NIT,
  17.  Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga – KASHWASA,
  18. Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma – MUWASA,
  19. Mamlaka ya Elimu na Mafunzo – VETA,
  20. Mahakama ya Rufaa Tanzania,
  21. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya – NHIF,
  22. Baraza la Taifa la Ujenzi - NCC
  23. Shirika la Umeme Tanzania, Kanda ya Mtwara,

 

Hivyo, tunapenda kuwaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaokuwa umejitokeza kutokana na makosa yaliyofanyika katika tangazo hilo. Kwahiyo, tangazo sahihi la kuitwa kazini mwezi Januari ni lililotoka upya tarehe 26 Januari, 2021 lenye jumla ya majina tisini (90), lenye Kumb. Na. EA.7/96/01/L/24.     

 

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Sekretarieti ya Ajira.

26 Januari,2021.