Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ipo katika mchakato wa Uboreshaji wa wa Mfumo wake wa maombi ya kazi “Recruitment portal “ ikiwa ni muendelezo wa uboreshaji wa utoaji huduma iliyo bora kwa wadau wake hususan watumiaji wa mfumo huo.
Kufuatia Maboresho hayo Sekretarieti ya ajira inawaalika wadau wake hususan waombaji kazi na watumiaji wa mfumo huo kuja kutoa maoni na ushauri wao utakaosaidia katika maboresho hayo kama sehemu ya wadau muhimu.
Waombaji kazi/watumiaji wa mfumo huo wanaoishi ndani ya Manispaa ya Morogoro wanaalikwa kuja kutoa maoni yao siku ya jumamosi tarehe 05 Desemba, 2020. Kikao cha upokeaji maoni kitaanza saa tatu kamili asubuhi katika kumbi za hotel ya Edema jirani na Chuo Kikuu cha Waislam (Muslim University).
Kupitia tangazo hili, wadau ambao wangependa kushiriki katika zoezi hilo muhimu watume majina yao kamili matatu, jinsia yao, ngazi ya elimu pamoja na utaalamu wa fani walizosomea na kutuma maombi yao kupitia barua pepe ya mfumo@ajira.go.tz kabla au ifikapo tarehe 03 Desemba 2020 saa tisa na nusu (9:30) mchana. Baada ya hapo kamati yetu iliyopangwa kupokea maoni ya wadau hao itachambua na kuchagua wadau 15 kwa kuzingatia Jinsi, uwakilishi wa kada kwa kila taaluma, ngazi za elimu pamoja uwakilishi wa Makundi maalum kama sehemu ya wawakilishi wa watumiaji wengine wa mfumo huo. Waombaji kazi wenye Taaluma za elimu na afya wanasisitizwa kujitokeza zaidi.
Aidha, kwa wale walioko nje ya Manispaa ya Morogoro na wangependa kutoa maoni, wanaombwa kutuma maoni yao kwa kutumia barua pepe maoni@ajira.go.tz kabla ya tarehe 04 Desemba, 2020.