TANGAZO KWA WASAILIWA WA KADA ZA TECHNICIAN-TANROAD NA TUTOR II (ICT)-WATER INSTITUTE(WI)

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, inapenda kuwataarifu Wasailiwa walioitwa kwenye Usaili kwa ajili ya Kada ya TECHNICIAN-TANROADS kuwa watafanya usaili  wa mchujo tarehe 16 Januari, 2020 badala ya tarehe 14 Januari, 2020 iliyokuwa imepangwa awali. Pia waombaji wa kada ya TUTOR II (ICT)-WATER INSTITUTE(WI) wanaarifiwa kuwa usaili wa mchujo wa kada hiyo utafanyika kwenye CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU DAR ES SALAAM(DUCE) . 

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na mabadiliko haya.