Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kujulisha waombaji kazi wote wa nafasi ya “AERONATICAL AIRPORT SERVICE OFFICER II” iliyotangazwa kwa niaba ya Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA) kuwa nafasi hiyo imesitishwa na hivyo maombi ya nafasi hiyo hayatoendelea kupokelewa kutokana na sababu zilizoelekezwa na mwajiri.
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza baada ya kutoa taarifa hii.
Kwa huduma mbalimbali au ufafanuzi tafadhali wasiliana nasi kupitia simu za kiganjani ambazo ni 0736-005511au 0735-398259 au 0784-398259.
Tangazo hili limetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
30 Disemba, 2020.