Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili utakaofanyika kwa njia ya Mtandao (OATS) Mkoa wa Ruvuma mnajulishwa kuwa kuna mabadiliko ya eneo la usaili.
Usaili utafanyika VETA- SONGEA badala ya Chuo cha Ualimu Songea kama ilivyoainishwa kwenye akaunti zenu za ajira portal. Muda na tarehe utabaki hivyohivyo kama ilivyoainishwa kwenye tangazo la kuitwa kwenye usaili.