TANGAZO LA KUWASISITIZIA BAADHI YA WASAILIWA WA NAFASI YA “CUSTOMS ASSISTANT II TRA”
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawasisitizia baadhi ya Wasailiwa wa nafasi ya Customs Assistant II wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wenye namba inayoanzia 1051-1583 wanatakiwa kwenda Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) tarehe 7/7/2020, Ukumbi “Lecture Theatre – A” saa 3:00 Asubuhi kwa ajili ya usaili wa kuandika.
Wasailiwa wengine wazingatie matangazo ya awali yalivyoelekeza kuwa tarehe 7/7/2020 kutakuwa na usaili wa Mchujo wa nafasi mbalimbali kwa kuzingatia sehemu waliyopangiwa na muda wa Usaili husika.
Isipokuwa kwa Usaili wa Mchujo wa nafasi ya “Personal Secretary” uliokuwa ufanyike tarehe 4 Julai, 2020 hautakuwepo na badala yake utafanyika usaili wa Vitendo tarehe 11 Julai, 2020 katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira, Kivukoni jijini Dar es Salaam.
Aidha, Sekretarieti ya Ajira inawaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kutokana na changamoto zilizo nje ya uwezo wetu.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Sekretarieti ya Ajira
06 Julai, 2020