TANGAZO LA KUHIMIZA KILA MSAILIWA KUNAKILI NAMBA YAKE YA USAILI

Kila Msailiwa mwenye usaili wa Mchujo au Vitendo anatakiwa kunakili namba yake ya usaili kwa usahihi aliyotumiwa kwenye akaunti yake katika mfumo wa maombi ya kazi wa Sekretarieti ya Ajira, namba ya usaili inaanza na PSRS/18/0639/43/ kutegemeana na nafasi aliyoiomba.

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawataarifu Wasailiwa wote walioorodheshwa katika tangazo lililotolewa tarehe 30 Julai, 2020 lenye Kumb.Na.EA.7/96/01/K/255 linaonyesha Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya “Land Transport Regulator Authority” (LATRA), “Tanzania Shipping Agencies Corporation” (TASAC), Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT), Chuo Kikuu cha Mzumbe (MU), Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA), “Livestock Training Agency” (LITA), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), “Tanzania Meteorology Authority” (TMA), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Shirika la Mzinga, Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) na “Institute of Accountancy Arusha” (IAA), anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili wa Vitendo unatarajiwa kufanyika tarehe 6 - 21 Agosti, 2020, usaili wa kuandika unatarajiwa kufanyika tarehe 08- 14 Agosti, 2020 na kufuatiwa na usaili wa mahojiano ambao utafanyika  tarehe 10-11 Agosti, 2020.

Wasailiwa ambao nafasi za kazi walizoomba zimeoneshwa kuwa watafanya Usaili wa Mchujo au Vitendo kuwa wanapaswa kuangalia katika akaunti zao walizotumia kujisajili kwenye mfumo wa maombi ya kazi na kuchukua namba ya usaili waliyotumiwa kwakuwa wataihitaji kuitumia kwenye saili husika. Kila Msailiwa anapaswa kuinukuu namba husika kwa usahihi kwa kuwa ndio namba itakayotumika kufanyia usaili na kupata matokeo ya usaili.

Pia, kila Msailiwa akumbuke kuvaa Barakoa siku ya usaili na kunawa mikono kila mara.

Tafadhali ukiona tangazo hili, mtaarifu na mwingine unayemfahamu anahusika kufanya usaili huo.

Limetolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Sekretarieti ya Ajira.

7 Agosti, 2020