KUONDOLEWA KWA BAADHI YA NAFASI ZILIZOTANGAZWA

KUONDOLEWA KWA BAADHI YA NAFASI ZILIZOTANGAZWA

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuujulisha Umma kuwa nafasi za kazi za kada mbili zilizoainishwa hapa chini zimeondolewa katika tangazo la awali na badala yake nafasi hizo zitajazwa kupitia Kanzidata (Database). nafasi hizo za kazi ni;-

  1. PERSONRAL SECRETARY II –       LATRA ,
  2. DRIVER III  - IAA 

Nafasi hizo zilitangazwa kwa niaba ya “Land Transport Regulator Authority” (LATRA) na “Institute of Accountancy Arusha” (IAA).  Tunawaomba radhi wadau wetu kutokana na usumbufu utakaojitokeza kutokana na marekebisho haya, hususani wale ambao waliwasilisha maombi ya kazi kwa ajili ya nafasi hizo, kwakuwa mchakato wake hautoendelea. Hivyo, wasisite kuwasilisha maombi yao ya kazi pindi nafasi hizo zikitangazwa tena katika ofisi yoyote ya Umma.

Kwa huduma mbalimbali au ufafanuzi tafadhali wasiliana nasi kupitia simu za kiganjani ambazo ni 0736-005511au 0735-398259 au 0784-398259.

           

Tangazo hili limetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

4 Agosti, 2020