TAARIFA KWA UMMA
Dar es Salaam, Desemba 5, 2020
TAARIFA YA KUHAMIA DODOMA KWA OFISI ZA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwafahamisha Watanzania na wadau wote kuwa makao makuu ya ofisi zake yamehamia Dodoma. Hivyo, kuanzia tarehe 15 Desemba, 2020 huduma mbalimbali kuhusu masuala ya uendeshaji wa mchakato wa ajira zitakuwa zinapatikana Dodoma katika majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) zilipo baadhi ya ofisi za Wizara mama (Utumishi) na eneo linalojulikana kwa jina la “Asha Rose Migiro Square”.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia anwani zifuatazo;-
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na
Eneo la“Asha Rose Migiro Square”.
S.L.P. 2320 - Dodoma
Simu: +255 22 2153517- 0735- 398259 – 0736-005511
Katibu@ajira.go.tz au gcu@ajira.go.tz au malalamiko@ajira.go.tz
www.ajira.go.tz
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Ghorofa ya tatu
Jengo la Sheria House- Mazizini
Au ilipo ofisi ya Kamisheni ya Wafu na Mali Amana (MAMBO MSIGE)
S.L.P. 1272 - Zanzibar.
Barua pepe: Zanzibaroffice@ajira.go.tz
Tunaomba radhi wadau wetu kwa usumbufu wowote utakaoweza kujitokeza.
Imetolewa na;-
Riziki V. Abraham
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.