MABADILIKO YA ENEO LA USAILI KWA WASAILIWA WA KADA YA AFISA HESABU II - DAR ES SALAAM

Usaili wa Kada ya AFISA HESABU II utafanyika katika ukumbi wa MAJOR GENERAL ISAMUHYO ULIOPO MGULANI JKT- DAR ES SALAAM.

Mabadiliko haya yanawahusu wasailiwa wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao wamepokea ujumbe kwenye Simu zao za Kiganjani na kwenye akaunti zao za Ajira Portal.

Aidha, muda na tarehe ya kufanyia usaili utabaki kama unavyoonekana katika tangazo la awali.