MABADILIKO YA MAHALI PA KUFANYIA USAILI WA KUANDIKA KWA NJIA YA MTANDAO (OATS) CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM)

Wasailiwa wote waliopangiwa kufanya usaili katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) – Dar es Salaam kwa tarehe 01 na 04 Novemba, 2024 mnajulishwa kuwa usaili wa Kuandika kwa njia ya mtandao ( online) kwa tarehe 01/11/2024 na tarehe 04/11/2024 utafanyika katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph (SJUIT) kilichopo Mbezi, Jijini Dar es salaam badala ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha ( IFM ) kama ilivyoonekana katika akaunti zenu hapo awali.