TANGAZO LA PILI LA USAILI WA MADEREVA

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Taasisi za Serikali, Wakala wa Serikali, Idara zinazojitegemea na Mamlaka za Serikali za mitaa, anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi ya (Dereva II) iliyotangazwa tarehe 29 Julai, 2019 ambao majina yao yako katika tangazo hili kuwa anatarajia kuendesha usaili wa Vitendo tarehe 31 Disemba, 2019 yatakayofanyika katika Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) jijini Dare es Salaam.

Majina ya wanaotakiwa kuhudhuria usaili tarehe 31 Disemba, 2019 yameambatishwa katika tangazo hili la kuitwa kwenye usaili kwa wale waliokidhi vigezo kwa mujibu wa tangazo la nafasi husika.

Aidha, Wasailiwa ambao majina yao yapo kwenye tangazo hili pamoja na yale yaliyopo kwenye tangazo la kuitwa kwenye usaili lililotoka tarehe 21 Novemba, 2019 kuwa saili zote za Vitendo zitafanyikia VETA jijini Dar es Salaam kulingana na ratiba zilizopo katika kila tangazo.

Kwa maelezo zaidi tembelea Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira www.ajira.go.tz  au piga simu namba 0736005511 kabla ya tarehe ya usaili kwa ufafanuzi zaidi.

Bofya hapa kuona majina ya kuitwa kwenye usaili-Dereva

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

25/11/2019

Attachments

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *