TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MSISITIZO

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Taasisi za Serikali, Wakala wa Serikali, Idara zinazojitegemea na Mamlaka za Serikali za mitaa, anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi ya (Dereva II) iliyotangazwa tarehe 29 Julai, 2019 kuwa anatarajia kuendesha usaili kwa waombaji 1617 wa nafasi hizo jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 03 hadi tarehe 30 Disemba, 2019.

Hivyo, kwa waombaji kazi walioomba nafasi ya udereva  katika Taasisi hizo za Umma waangalie  majina ya kuitwa kwenye usaili kwa wale waliokidhi vigezo kwa mujibu wa tangazo la nafasi husika ili kujiandaa kufanya usaili kulingana na nafasi na tarehe aliyopangiwa.

Ili kufahamu taarifa sahihi ya Tangazo hilo  tembelea Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira  www.ajira.go.tz  au piga simu namba 0736005511 kabla ya tarehe ya usaili kwa ufafanuzi zaidi.

 Bofya hapa kuona majina ya walioitwa kwenye usaili

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

21/11/2019

 

Attachments

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *