TANGAZO LA MSISITIZO WA KUITWA KAZINI

JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

TANGAZO LA KUITWA KAZINI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa umma anapenda kuwatangazia waombaji kazi waliofanya saili Wizara, Mamlaka, Taasisi mbalimbali, Wakala za Serikali, Idara zinazojitegemea, Mashirika ya Umma, Sekretariti za Mikoa na Halmasahauri mbalimbali kuwa ametoa tangazo la kuwaita kazini  tarehe 2 Novemba 2019 kwa wasailiwa 670 waliofaulu saili hizo na kuwapangia vituo vya kazi katika maeneo mbalimbali ikiwemo;-

 Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ,  Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Madini, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  Wizara ya Nishati.

Maeneo mengine waliyopangiwa ni  kwenye Mamlaka, Tume, Bodi,  Mashirika, Kampuni pamoja  na Taasisi mbalimbali ya umma ikiwemo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),  Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA),  Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), Tume ya Madini (TMC), Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB),  Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),  Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC),  Kampuni ya Huduma za Meli-Mwanza, Bohari ya Dawa (MSD), Kituo cha Zana za Kilimo na Ufundi Vijijini (CAMARTEC) Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) na  Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD),

Wasailiwa wengine waliofaulu wamepangiwa kwa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD), Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA),Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA),   Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA), Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) na Wakala wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT).

Wengine wamepangiwa katika Vyuo vya Elimu ikiwemo, Chuo Kikuu Cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT), Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Chuo cha Bahari cha Dar Es Salaam (DMI), Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Chuo cha Uhifadhi Wanyamapori (MWEKA) na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM).

Sehemu nyingine walikopangiwa ni Ofisi za Wakuu wa Mikoa ya Arusha, Mtwara, Mwanza, Songwe na mkoa waTabora. Wengine wamepangiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Morogoro, Moshi, Mpanda, Mtwara – Mikindani, Songea na Manispaa Temeke,Nyingine ni pamoja na Halmashauri za jiji la Arusha, Dodoma, Tanga na jiji la Mwanza. Wengine wamepangiwa katika Halmashauri ya Mji wa Handeni, Mafinga, Kibaha, na Mji wa Tunduma. Ilihali wengine wamepangiwa katika Halmashauri ya Wilaya za Busega, Bahi, Chemba, Buchosa, Mbulu, Handeni, Itilima, Kibaha, Kisarawe, Kondoa, Lindi, Magu, Makete, Maswa, Mbeya, Mbogwe, Meatu, Misungwi, Mtwara, Muheza, Mvomero, Mbalali, Sumbawanga, Ushetu pamoja na Wilaya ya Urambo.

Wasailiwa wote wanapaswa kwenda kuchukua barua zaowakiwa na kitambulisho katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira kuanzia tarehe 7 Novemba, 2019 ili kuweza kwenda kuripoti kwa waajiri waliopangiwa kwa wakati. Aidha, kwa watakaoshindwa kwenda kuchukua barua zao ndani ya siku saba barua hizo zitatumwa kupitia masanduku yao ya Posta. Aidha, ili kupata taarifa zaidi ikiwemo majina ya wasailiwa waliofaulu na kupangiwa vituo vya kazi pamoja na matangazo mbalimbali ya nafasi za kazi tembelea Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira www.ajira.go.tz  eneo la Placement au piga simu namba 0736005511 kwa ufafanuzi zaidi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

06/11/2019

Attachments

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *