TANGAZO KWA WASAILIWA WA NAFASI MBALIMBALI SERIKALINI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anawatangazia Wasailiwa wote wanaotakiwa kufanya usaili wa Mchujo katika kada mbalimbali zilizotangazwa kuanzia tarehe 10/09/2019 kwa ajili ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na Tangazo lililotoka tarehe 13/9/2019 la Ofisi mbalimbali za Umma na kuendelea kuwa ni Marufuku kwa Msailiwa yeyote kuja/kuingia na Simu ama kifaa chochote cha kunakili taarifa/ matukio katika chumba cha usaili wa mchujo.

Aidha, Wasailiwa wote wanapaswa kuwa/kukumbuka ama kuandika mahali taarifa zifuatazo;-

  1. Kufahamu (Serial number) yenye jina lake kama ilivyo kwenye tangazo la nafasi ya kazi husika.
  2. Kufahamu tarehe ya usaili husika kama ilivyo kwenye tangazo.
  • Kujua sehemu/eneo atakalofanyia usaili kama ilivyoainishwa kwenye tangazo husika.
  1. Kuja na nakala halisi za Vyeti vyake vya kitaaluma au nyaraka nyinginezo muhimu kulingana na taaluma yake.
  2. Kuwa na kitambulisho kimojawapo cha kumtambulisha kati ya hivi:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha Kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;
  3. Kuvaa mavazi yenye staha.
  • Kufika kwa wakati katika sehemu za kufanyia saili kulingana na muda ulioainishwa kwenye matangazo husika.

Kwa msailiwa yeyote atakayeshindwa kufuata taratibu hizo hatua zaidi zitachukuliwa ikiwemo kuondolewa katika mchakato wa kuipata nafasi ya kazi aliyoiomba.

Mwisho, ili kufahamu taarifa sahihi ya matangazo hayo tembelea Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira www.ajira.go.tz au piga simu namba 0736005511 kabla ya tarehe ya usaili.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *