TANGAZO LA KUITWA KAZINI WAOMBAJI KAZI 337

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Waajiri wa Ofisi mbalimbali za Umma, inapenda kuwafahamisha wadau wake ambao wamekuwa wakifuatilia Matangazo ya fursa za Ajira serikalini kuwa imetoa tangazo la kuwaita kazini waombaji kazi waliofaulu katika saili mbalimbali wapatao mia tatu thelathini na saba (337).

Tangazo hilo la kuwaita kazini limetoka tarehe 15 Agosti, 2019 katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira waangalie sehemu ya (Placement).

Waombaji hao wamepangiwa katika takribani Ofisi arobaini (40) za Umma, ikiwemo Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Halmashauri za Wilaya,  Halmashauri za Mji, TCAA, TRA, TRC, TAWA, MOI, TCB, UDSM, TBT, ORCI,CBE, MSD, TVLA, TICD, BRELA na taasisi nyinginezo.

Kwa maelezo zaidi ya tangazo hili na mengine tafadhali tembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kupitia www.ajira.go.tz au waweza kupiga simu namba, 0736-005511.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

15 Agosti, 2019

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *