TANGAZO LA KUITWA KAZINI TANESCO

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwafahamisha wadau wake ambao wamekuwa wakifuatilia Matangazo ya fursa za Ajira za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuelewa kuwa imetoa matangazo ya aina tatu kwa ajili ya TANESCO kama ifuatavyo:-

  1. Kuna Tangazo la kuitwa kazini kwa Waombaji wa fursa za Ajira mia sitini na mbili (162) ambalo limetoka tarehe 10 Agosti, 2019 likiwataka wahusika walioainishwa katika tangazo hilo kuripoti kazini TANESCO mara baada ya kupata barua za kupangiwa kituo cha kazi.

 

  1. Kuna Tangazo la kuitwa kwenye usaili kwa Ajira za Muda Maalumu mia moja tisini na saba (197) kwa Waombaji waliokidhi vigezo lililotoka tarehe 6 Agosti, 2019 kwa niaba ya  Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Kati Dodoma ambalo usaili wake  umepangwa kufanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma kuanzia tarehe 14 hadi 17 Agosti, 2019.

 

  • Tangazo lingine ni za nafasi wazi za kazi mia tano sitini na tisa (569) kwa ajili ya Shirika hilo hilo la TANESCO lililotoka tarehe 31 Julai, 2019 ambalo mwisho wa kupokea maombi yake ya kazi ni tarehe 13 Agosti, 2019 bado nafasi hizo ziko wazi, hivyo, wanahimizwa Watanzania wenye sifa waendelee kutuma maombi ya kazi ili waweze kuajiriwa serikalini.

 

Kwa maelezo zaidi ya matangazo haya na mengine tafadhali tembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kupitia www.ajira.go.tz au waweza kupiga simu namba, 0736-005511.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

13 Agosti, 2019

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *