TANGAZO LA KUITWA KAZINI TPA

Sekretarieti ya Ajira kwa niaba ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inawataka Waombaji wa fursa za Ajira waliokuwa wamefanya Usaili kwa ajili ya TPA kuwa imewaita kazini waombaji mia tatu (300) waliofaulu usaili husika, hivyo wanapaswa kuangalia majina yao kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira pamoja na Tovuti ya TPA.Aidha, wote watakaoona majina yao, wanapaswa kufika mara moja katika Ofisi za TPA Makao Makuu (Bandari Tower) ghorofa ya 32 kwa ajili ya kuchukua barua zao na kupewa maelekezo mengine ya msingi.

Kwa maelezo zaidi ya matangazo haya na mengine tafadhali tembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kupitia www.ajira.go.tz au www.ports.go.tz pia waweza kupiga simu namba, 0736-005511.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

9 Agosti, 2019

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *