TANGAZO KWA WAOMBAJI WA FURSA ZA AJIRA TANESCO

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwafahamisha
wadau kuwa tangazo la nafasi wazi za kazi kwa ajili ya Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) lililotoka tarehe 31 Julai, 2019 ambalo mwisho wa kupokea maombi yake
ya kazi ni tarehe 13 Agosti, 2019 bado hizo nafasi ziko wazi.
Hivyo, tangazo la kuita kwenye usaili Waombaji waliokidhi vigezo lililotoka tarehe 6
Agosti, 2019 lilikuwa limetolewa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya
Kati Dodoma mnamo mwezi Aprili mwaka huu, ambapo usaili wake ndio umepangwa
kufanyika kuanzia tarehe 14 hadi 17 Agosti, 2019 jijini Dodoma katika viunga vya
Chuo Kikuu cha Dodoma.
Kwa maelezo zaidi tembelea www.ajira.go.tz au piga simu namba, 0736-005511.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *