Msemaji Mkuu wa Serikali akutana na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbas amemtembelea ofisini kwake leo, Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi ikiwa ni muendelezo wa ziara za kikazi za Dkt Abbas katika ofisi mbalimbali.

Katika mazungumzo yao pamoja na mambo mengine Dkt. Abbas amesema lengo la ziara yake ni kujifunza na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali kati yao  ili kuendelea kuimarisha mahusiano na mashirikiano ya kikazi.

Dkt. Abbas alifafanua kuwa ili kuweza kuisema Serikali kwa mapana yake ni lazima kuzitembelea ofisi mbalimbali na kukutana na Viongozi pamoja na kujionea mazingira halisi ya kazi, ili anapozungumza jambo fulani anakuwa analifahamu na si kwa kuhadithiwa.

Kwa upande wake, Katibu wa Sekretarieti ya Ajira amemshukuru kwa uamuzi wake wa kumtembelea na kumuahidi kuendelea kumpa ushirikiano wakati wote, kwakuwa yeye anaamini ofisi ya msemaji Mkuu wa Serikali ni nafasi muhimu na ndio maana Serikali ikaipa uzito ili wananchi waweze kupata taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu Serikali yao.

Sambamba na hilo, Katibu  alimweleza Dkt. Abbas kuwa Ofisi yake katika  kuendelea kusogeza huduma karibu na wadau wake imeanzisha mfumo wa maombi ya kazi unaojulikana kama (recruitment portal) ambao umegawanyika katika sehemu tatu, sehemu ya Mwajiri, sehemu ya Sekretarieti ya Ajira na sehemu ya Waombaji wa kazi.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxmwishoxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *