WATUMISHI WA SEKRETARIETI YA AJIRA WATAKIWA KUTAMBUA DHAMANA WALIYONAYO

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi amewataka watumishi wa taasisi yake kujiepusha kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadili kwa kuwa wao ni kioo cha wale wanao wa hudumia hususani vijana wanaotafuta kazi serikalini.

Amesema hayo wakati wa kikao kazi cha kutathimini namna Ofisi yake ilivyoendesha saili zilizopita ikiwemo zile ziizokasimiwa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa na pamoja na baadhi ya vyuo mbalimbali nchini.

Katibu huyo, amewasisitiza watumishi hao, kuwa hatakuwa tayari kumvumilia mtumishi yeyote atakayethibitika kwenda kinyume cha Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma na kujihusisha na vitendo vya rushwa ama matumizi mabaya ya nafasi aliyonayo ndani ya taasisi.

“Napenda muelewe jukumu tulilokabidhiwa la kuendesha mchakato wa ajira kwa niaba ya Waajiri, ni jukumu nyeti linalogusa maisha ya watu. Pia inaonyesha tumeaminiwa, hivyo tunapaswa kutimiza wajibu wetu kwa kuzingatia misingi ya haki, uwazi, maadili na si vinginevyo” amesema Daudi.

Kikao hicho cha tathimini kimefanyika baada ya ziara ya kikazi aliyofanya Katibu huyo katika mikoa 12 ya Tanzania Bara ambapo aliweza kukutana na waajiri pamoja na Bodi za Ajira katika halmashauri 19 ndani ya mikoa hiyo aliyoweza kutembelea mpaka sasa.

Ambapo ameainisha kuwa lengo la ziara yake ilikuwa ni pamoja na kupata mrejesho kutoka kwa Waajiri ikiwemo kufahamu namna saili zinavyofanyika, ubora wa watumishi wanaopatikana na ushirikiano wa kikazi wa watumishi wa Ofisi yake wanapo mwakilisha katika Ofisi hizo.

 

XXXXXXXXXXXXXXXXXXMWISHOXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *