TANGAZO LA WASAILIWA WA NAFASI YA KAZI YA UDEREVA NA ASSISTANT ACCOUNTANT

Sekretarieti ya Ajira inapenda kuwataarifu wasailiwa wote walioomba nafasi ya kazi ya Udereva kwa ajili ya MDA’s na LGA’s kuwa usaili kwa vitendo utafanyika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Chang’ombe Jijini Dar es Salaam.
Aidha, kwa waombaji walioitwa kwenye usaili kwa nafasi ya kazi ya Assistant Accountant kwa ajili ya Tanzania Veterinary Laboratory Authority (TVLA), usaili wao utafanyika Chuo cha Mwalimu Nyerere Kigamboni badala ya Dar es Salaam University College (DUCE).
Tarehe za usaili ni kama zilivyoainishwa katika tangazo la kuitwa kwenye usaili lililotolewa awali.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
5 Julai, 2019

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *