MATOKEO YA USAILI WA VITENDO KADA ZA VETA ULIOFANYIKA TAREHE 11,12 NA 13 FEB, 2019

MATOKEO YA PRACTICAL VETA

6 Comments

 1. erick nm.

  kwanini msifungue matawi kwa kanda yan unakuta nafasi zinazoombwa labda ni kwa ajili ya mkoa wa arusha lakini tume ya ajira mnaitisha watu wengi na nafasi ni chache,huu ni ushauri wangu tu mana nafasi mojamnaita watu elf tatu au watu mia sita fanyeni taratibu mfungue ofisi za kanda na zifanye kazi kama nyie mnawaumiza na kuwatesa wanaotoka mbali sio kila mtu anandugu dares salaam.

  Reply
  1. PSRS (Post author)

   Habari Erick, Tumeanza kufungua ofisi za Kanda kwa kuanzia Zanzibar na Muda si mrefu ofisi zetu zitahamia Dodoma, nia yetu ni kuendelea kusogeza huduma karibu na wateja wetu, Hata hivto maombi yanapokuwa mengi kutoka kwa waombaji wetu huwa tunajitahidi kufanya usaili kikanda pale bajeti inaporuhusu, Kuhusu kuitwa waombaji wengi kwa nafasi chache tunapenda kukuarifu kuwa Matangazo yetu yanakuwa kwa uwazi na inamuwezesha kila mwenye sifa kwa mujibu wa tangazo kuomba na kuitwa kwenye usaili kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu.

   Reply
 2. Crotilda prosper domisian

  Nimehudhuria usaili kama tangazo lilivyoelekeza lakini kulikuwa na shida kidogo maana wasimamizi walidai hatukuitwa hadi tulipowaonesha tangazo. Baada ya mda kidogo tulipewa huo usaili wa vitendo. Cha kushangaza leo matokeo yametoka kwa ajili ya usaili mwingine hatuoni matokeo. Hii inafedhehesha sana. Kada ni Vocational teacher design sewing and cloth technology.

  Reply
  1. PSRS (Post author)

   Pole Crotilda kwa changamoto hiyo, Tunashukuru kuwa tulitatua changamoto hiyo na kada hiyo mlikuwa wawili na wote mlifanyiwa usaili kwa wakati, Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwenu

   Reply
 3. DEUSDEDITH MKILINDI MSUNGO

  Baba /mama/kaka/dada shikamo, natumaini nyote mpo salama. Nashukuru kwa weledi wenu wa kutuwekea portal za kazi. Hakika ni ubunifu mzuri sana sana. Nawashukuru sana sana. Nawapongeza kwa huduma nzuri manzotupa na mzidi kutupa zaidi.

  Mimi nina utaalamu kwenye tasnia ya afya ya mifugo na uzalishaji kutoka katika Chuo Kikuu cha SUA. Naomba pia kama mnaweza pia kutulea nafasi mbalimbali katika sekta ya mifugo na uvuvi.

  Pia binafsi unaweza kuniunganisha hata kwenye makampuni ambayo naweza kujitolea na kwenye halmashauri mbalimbali hapa nchini. Naomba sana ndugu zangu.

  Natumaini ombi langu utanisaidia ,asante sana na Mungu awabariki sana.

  Mawasiliano 0754465430
  Email deusdedithmsungo1@gmail.com.

  Asante sana .

  Reply
  1. PSRS (Post author)

   Tunashukuru kwa pongezi ndugu Mkilindi, na pongezi kwako kwa kuhitimu mafunzo yako SUA, Sekretarieti ya Ajira itakapopokea vibali vya kada hizo zitatangazwa kwa uwazi.
   Aidha kwa sasa Sekretarieti ya ajira haina utaratibu wa kuwaunganisha wahitimu kwenye makampuni binafsi au Halmashauri, Tunakushauri kuwasiliana na Taasisi nyingine kama Wakala wa Huduma za Ajira ili uweze kupata muongozo zaidi wa suala lako.

   Reply

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *