TAARIFA YA KUWAALIKA WATUMIAJI WA MFUMO WA AJIRA KUTOA MAONI YA UBORESHAJI WA MFUMO HUO.

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ipo katika mchakato wa Uboreshaji wa wa Mfumo wake wa maombi ya kazi “Recruitment portal “ ikiwa ni muendelezo wa uboreshaji wa utoaji huduma iliyo bora kwa wadau wake husasuan watumiaji wa mfumo huo.

Kufuatia Maboresho hayo Sekretarieti ya Ajira inawaalika wadau wake hususan waombaji kazi na watumiaji wa mfumo huo kuja kutoa maoni na ushauri wao utakaosaidia katika maboresho hayo kama sehemu ya wadau muhimu.
Waombaji kazi/watumiaji wa mfumo huo wanaalikwa kutoa maoni yao siku ya jumatano tarehe 19 na siku ya Alhamis tarehe 20 Desemba, 2018 katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira ambazo zimehamia Jengo la Utumishi House Magogoni kuanzia saa tatu kamili asubuhi.

Wadau ambao wangependa kushiriki katika zoezi hilo muhimu wanapaswa kutuma majina yao kamili matatu, jinsi yao, utaalamu wa fani walizosomea, namba zao za simu na kutuma maombi taarifa hizo kupitia barua pepe ya mfumo@ajira.go.tz kabla au ifikapo tarehe 18 saa sita na nusu (6:30) mchana, Baada ya hapo kamati yetu iliyopangwa kupokea maoni ya wadau hao itachambua na kuchagua wadau 50 kwa kuzingatia Jinsi, uwakilishi wa kada kwa kila taaluma, ngazi za elimu pamoja uwakilishi wa Makundi maalum kama sehemu ya wawakilishi wa watumiaji wengine wa mfumo huo.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Ajira
Tarehe 17 Desemba, 2018.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *