TANGAZO KWA WAOMBAJI KAZI

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwajulisha waombaji kazi wote kuwa, wanatakiwa kuhakikisha taarifa wanazoingiza katika mfumo wa Maombi ya kazi (Recruitment portal) zinafanana na taarifa walizojaza wakati wa kujiandikisha ili kupatiwa vitambulisho vya Uraia kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Lengo la zoezi hili ni kuhakikisha kuwa, waombaji kazi wanakuwa na taarifa zinazofanana na taarifa zao katika taasisi nyingine. Taarifa hizi ni pamoja na majina kamili, umri wa mhusika, mahala ulipozaliwa, anuani na taarifa nyingine zinazoendana na hizo.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Ajira.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *