Majibu ya hoja na maoni ya wadau kwa mwezi Julai, 2018.

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inaendelea kuwashukuru wadau na wananchi mbalimbali wanaotuandikia maoni pamoja na kuuliza maswali mbalimbali yanayohusu Ajira kwa kipindi cha mwezi Julai,2018. Wale wote waliotuandikia maoni na maswali yao kupitia barua pepe na kurasa zetu za ‘facebook’ na ‘Instagram’ tumeendelea kuwapa majibu ya hoja zao kadri wanavyouliza.

Aidha kwa maswali yanayofanana na yanayohitaji uelewa wa jumla tumeyaunganisha na kuyatolea majibu kwa faida ya wasomaji wetu wengine ili kuendelea kutoa elimu kuhusu masuala yanayohusu Uendeshaji wa Mchakato wa Ajira Serikalini.

Swali la kwanza.

Je fursa za Walemavu katika mchakato wa Ajira kwa mujibu wa Sheria zinavyozingatiwa?

Jibu.

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inasimamia Sheria, Kanuni na Taratibu katika kutekeleza mchakato wa Ajira Serikalini.

Sheria ya Walemavu Sura 183, Kifungu cha 33 (1) kimeeleza wazi utaratibu unaotakiwa kufuatwa wakati wa kutekeleza mchakato wa Ajira ndani ya Utumishi wa Umma. Sambamba na Sheria hiyo pia Kanuni za Uendeshaji za Sekretarieti ya Ajira za mwaka 2009, Kanuni ya 16 (1) imeainisha wazi wastani anaotakiwa kufikia kila msailiwa ili aweze kuajiriwa kuanzia madaraja ya kuingilia, nafasi za Wanataaluma hadi ngazi ya Watendaji Wakuu.

Kwa kuzingatia msingi huo, Sekretarieti ya Ajira imeweka wazi katika mfumo wake wa uwasilishaji wa maombi ya kazi ikiwataarifu waombaji wa fursa za

Ajira kuainisha katika mfumo na hata kueleza kwenye barua endapo ni mlemavu ili kwanza kuweza kumwandalia mazingira rafiki kulingana na hali yake ili aweze kufanya usaili bila ya matatizo. Sambamba, na hilo pindi inapotokea kuna mlemavu aliyefanya usaili na kufikia wastani unaotakiwa na kufungana na wasailiwa wengine basi msailiwa mwenye ulemavu hupewa kipaumbele cha kupata Ajira.

Swali la pili.

Napenda kufahamu ni namna gani naweza kupata mrejesho baada ya kutuma maombi ya kazi kupitia mfumo wa ajira.

Jibu.

Maboresho yaliyofanyika katika mfumo wa ajira kwa sasa yanampa mrejesho wa aina mbili (2) mwombaji kazi kama ifuatavyo;

Mrejesho wa kwanza ni pale mwombaji anapoomba kazi ambayo hakustahili kuiomba kutokana na sifa zilizopo katika tangazo. Mfumo hautamruhusu kuomba kazi hiyo na utampa sababu ya kutokustahili maombi yake kupokelewa. Mfano, endapo tangazo linamhitaji mwombaji kazi mwenye umri chini ya miaka 45, wale wote ambao umri umezidi hawataruhusiwa kuomba na mfumo utawapa sababu ya kutokubaliwa kuomba kazi hiyo kwa kuwa na umri mkubwa au kama nafasi ya kazi iliyotangazwa inahitaji mtu mwenye elimu ya kiwango cha Astashahada endapo ataomba mtu mwenye kiwango cha elimu tofauti na hicho mfumo pia utampa sababu ya kutokubaliwa.

Pili, mrejesho kupitia akaunti ya mfumo na barua pepe (email). Katika hatua hii mwombaji kazi baada ya kufanikiwa kuomba kazi, atakuwa anapokea mrejesho kulingana na hatua “stage” ya usaili iliyopo. Mathalani, akiomba kazi na kufanikiwa, mfumo utamtumia barua pepe ukimjulisha kuwa maombi yako yamefika na akichaguliwa ‘shortlisted’ mfumo utamjulisha kuwa amechaguliwa kwa hatua nyingine na hata anapofaulu usaili, mfumo una uwezo wa kumjulisha kuwa amefaulu usaili.

Swali la tatu

Kumekuwa na uelewa tofauti kwa baadhi ya waombaji kazi kuhusu asilimia anazopaswa kuwa nazo mwombaji wa ajira pindi ajazapo taarifa zake katika mfumo, je mnaweza kutoa ufafanuzi katika hili.

Jibu

Tungependa kuwajulisha waombaji fursa za Ajira kuwa, Mfumo wa maombi ya kazi unamhitaji mwombaji aingize taarifa za msingi ambazo hazina tofauti na zile anazoweka katika wasifu wake binafsi (CV). Kinacho ongezeka ni ushahidi wa taarifa zake ambapo vyeti husika pia huingizwa katika mfumo.

Mwombaji kazi kabla hajaanza kuingiza taarifa zake, mfumo humpatia ASILIMIA 0 ya taarifa zake. Anapoanza kuingiza taarifa, mfumo huongeza alama (katika asilimia) za kiwango cha taarifa alizoingiza. Mwombaji anapofikisha kuanzia asilimia 75 ya taarifa zake, mfumo humruhusu kuomba kazi. Sekretarieti ya Ajira tunaamini kuwa taarifa za mwombaji zinapofikia kiwango cha ASILIMIA 75, taarifa zake zinakuwa zinajitosheleza kumfahamu vizuri na hivyo tunampa nafasi ya kuomba nafasi za kazi kupitia mfumo huo unaopatikana kwa anuani ya http://portal.ajira.go.tz

Aidha ni muhimu kutambua kuwa, kuingiza taarifa kwenye mfumo wetu wa maombi ya kazi kwa asilimia zaidi ya 75, hakumfanyi mwombaji kuamini kuwa tayari ameomba kazi, bali atambue kuwa taarifa zake zimejitosheleza na hivyo anayo fursa ya kuomba kazi kupitia mfumo wetu endapo nafasi za kazi zimetangazwa.

Ni muhimu pia kufahamu kuwa mfumo huu umejengwa kwa kuzingatia elimu za wahusika, Kwa maana kuwa hata mwenye Elimu ya kidato cha nne na

astashahada anaweza kuomba kazi kwani aingizapo

Swali la nne.

Je ni kweli kuwa maboresho ya Mfumo yamesaidia kupunguza muda wa mchakato wa ajira?.

Jibu.

Maboresho katika mfumo wa maombi ya kazi umesaidia sana Sekretarieti ya Ajira na Serikali kwa ujumla kupata watumishi wenye sifa kwa wakati. Kwa upande wa Sekretarieti ya Ajira, maboresho haya yamesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza muda wa mchakato wa Ajira. Kabla ya mfumo huu kuanza, mchakato wa ajira ulichukua siku 72 hadi 90 kuanzia kutangaza nafasi za kazi hadi kupangia kazi waliofaulu, lakini kwa sasa tunatumia siku 52 na nimatumaini yetu kuwa muda huu utapungua zaidi. Lengo ni kufikia siku 42 ama pungufu ya hapo. Pia, maboresho haya yameufanya mfumo uweze kubaini waombaji kazi ambao hubadilisha taarifa zao ili kuomba kazi. Baada ya maboresho, mfumo unaweza kuweka kumbukumbu ya kila badiliko linalofanywa na mwombaji kupitia akaunti yake na hivyo ni rahisi kuwabaini waombaji kazi wadanganyifu.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

13 Comments

 1. Japhet

  Naomba nijue,mfano cheti cha utambulisho wa usajiri kutoka bosi ya ugavi na manunuzi,tunaattach kwenye kipengele kipi.
  Other attachment au wap.

  Pili,kwenye kifungu cha other attachment kuna kipengele cha CV,lkn mfumo unatoa fursa ya kutengeneza CV.JE nimuhimu sana kuweka CV yangu,na mboa nikiweka mfumo unakataa.

  Reply
  1. admin

   Habari Japhet;
   1. Cheti cha utambulisho wa usajiri kutoka bodi ya ugavi na manunuzi utaweka upande wa ‘Professional Qualification’

   2. Taarifa unazojaza katika mfumo ni CV yako, isipokuwa kama una CV ambayo ni kubwa kuliko hizo taarifa unazojaza unaweza kuweka CV yako upande wa ‘Other Attachment’ na Cv yako isizidi 2MB.

   Reply
 2. peter

  kwa mtu aliyepotelewa na vyeti anasaidiwa vipi ili nafasi za ajira zisimpite

  Reply
  1. admin

   Habari Peter,
   kama umeripoti upotevu wa vyeti vyako na NECTA wametuma taarifa zako Sekretarieti ya Ajira basi utakuwa na uwezo wa kuomba nafasi za kazi zitakazokuwa zinatangazwa kupitia ‘Recruitment Portal’, MFANO: ukifungua ‘profile’ yako upande wa ‘Academic Qualification’ sehemu ya ‘Education level’ utakuta ‘Ordinary Level’ utaona sehemu imeandikwa ‘Click here if you have lost your certificate’ halikadhalika kwa ‘Advanced level’
   Nakutakia kila la Kheri!

   Reply
 3. Edwin Bishanga

  Nauliza hivi mmetanabaisha kuwa mkitangaza kazi mpaka kupata waajiriwa mnatumia almost siku 52 mbona kuna kazi nyingine mnatangaza almost sasa ni siku ya 50 na hamjaita hata usaili!?

  Reply
  1. admin

   asante kwa swali lako, Ni nafasi zipi ambazo ulituma maombi kwa zaidi ya siku 50 sasa bado hawajaitwa kwenye usaili?

   Reply
  2. admin

   asante kwa swali lako, Ni nafasi zipi ambazo ulituma maombi kwa zaidi ya siku 50 sasa bado hawajaitwa kwenye usaili?

   Reply
   1. Edwin Bishanga

    Tanzania Airports Authority. Assistant security officer.

    Reply
 4. Mudhihiri Mwinyi

  Habari,kwa nini affidavity isiwe mbada wa cheti cha kuzaliwa kwani affidavity haipo kwa mujibu wa sheria?

  Reply
  1. admin

   Salama Ndugu mwinyi, kama huna cheti cha kuzaliwa haiwezi kuwa sababu ya kutokuitwa kwenye usaili au kuomba nafasi za kazi zinapotangazwa, kwa wale ambao hawajapata cheti cha kuzaliwa Affidavity pia inakubalika

   Reply
 5. Abdul

  Je kwa Dereva alie na leseni class E na C na alisoma Certificate katika ngazi ya chuo hajawahi patwa na ajali na uzoefu zaidi ya miaka 8 iila HANA CHETI CHA TEST TRADE 2, ni kwa nini hawapati ajira na je hiko cheti cha mechanical trade test kinatolewa wapi?

  Reply
  1. admin

   Cheti cha TRADE Test II Kinatolewa VETA, Aidha zipo nafasi za Dereva ambazo huwa zinatangazwa bila Sharti la Trade Test II hivyo tunakushauri kutembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira http://www.ajira.go.tz

   Reply
 6. Edwin Bishanga

  Niliuliza swali tar 18 October 2018 nafasi za kazi mlizotangaza za Assistant security officer muajiri akiwa ni Tanzania Airports Authority (TAA) ziliishia wapi!? Maana kwa mujibu wa utaratibu mliojiwekea kwamba mnafuata mpaka sasa mko nje ya utaratibu huo.

  Reply

Leave a Reply to admin Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *