Call for Interview

Placements

Visitors Counter

»Online   4        
»Today   21       
»Yesterday  3474       
»Week   3495        
»Month   13958       
==================
»Total 20732919        

MAJIBU YA MASWALI NA HOJA ZA WADAU ZILIZOPOKELEWA MWEZI OKTOBA, 2016

Posted on November 17, 2016 at 10:07 AM

Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwashukuru Wadau wake na wananchi wote kwa ujumla waliotembelea tovuti (www.ajira.go.tz), waliofika ofisini kuonana na Maafisa kupata ufafanuzi wa maswala mbalimbali, waliopiga simu, waliotuma barua pepe na kutuandikia maoni pamoja na kuuliza maswali kwa kipindi cha mwezi Oktoba, 2016.

Hoja tulizozipokea kwa njia zote zilizoainishwa hapo juu   zimejumuishwa na kutolewa majibu ya jumla kwa hoja zinazofanana kwa faida ya wadau wote ili kuendelea kuelimisha umma kuhusu masuala ya Uendeshaji wa Mchakato wa Ajira Serikalini, majibu binafsi pia yametumwa kwa wadau wote waliotuma hoja zao mahsusi na maoni katika njia walizozitumia.

Read More

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Posted on October 1, 2016 at 07:09 PM

KUKANUSHA TAARIFA YA TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZAIDI YA 1000 SERIKALINI LILILOSAMBAA MITANDAONI

Kama mnavyofahamu hivi karibuni Serikali ilitoa taarifa ya kusitisha kwa muda Ajira mpya Serikalini kwa ajili ya kupisha zoezi la uhakiki wa Watumishi wake pamoja na zoezi la kupitia upya miundo yake, mazoezi haya mpaka sasa yanaendelea na hayajakamilika hivyo zoezi la usitishwaji wa Ajira bado linaendelea. 

 

Read More

KUKANUSHA TAARIFA KUHUSU TANGAZO LA AJIRA SERIKALINI

Posted on September 30, 2016 at 07:05 PM

Kuna tangazo ambalo linasambazwa kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii lenye kichwa cha habari ‘’Sekretarieti ya Ajira yatangaza zaidi ya nafasi za kazi 1,000’’. Likionyesha kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 1,101 kwa niaba ya waajiri mbalimbali Serikalini.

Read More

Wajumbe wa Bodi ya zabuni wapewa semina ya mabadiliko ya Sheria ya Ununuzi wa Umma.

Posted on August 19, 2016 at 07:10 PM

Wajumbe wa Bodi ya zabuni na Menejimenti ya Sekretarieti ya Ajira wamepata mafunzo kuhusiana na mabadiliko ya sheria ya ununuzi wa Umma namba 5 ya mwaka 2016 ili kuwajengea uwezo wa kuendana na mabadiliko hayo katika ununuzi wa Umma.

Read More

Taarifa kwa Umma.

Posted on August 9, 2016 at 08:27 PM

Hivi Karibuni Serikali ilitoa taarifa kwa umma kuwa Ajira zimesitishwa kwa muda ili kupisha zoezi linaloendelea la uhakiki wa watumishi Serikalini. Aidha Sekretarieti ya Ajira pia ilitoa taarifa ya kuahirishwa kwa usaili wa nafasi za kazi kwa tangazo lililotolewa tarehe 1 Juni, 2016 hadi hapo mtakapoarifiwa tena.

Read More