MPANGILIO WA USAILI WA MCHUJO (WRITTEN INTERVIEW) WA KADA ZA TRA UTAKAOFANYIKA KATIKA KANDA 10.

August 23, 2017


Waombaji kazi waliochaguliwa kwa ajili ya usaili wa Mchujo wa nafasi mbalimbali za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zilizotangazwa hivi karibuni wanataarifiwa kuwa usaili wa hatua ya mchujo utafanyika katika Mikoa/kanda 10 kuanzia tarehe 30, 31 Agosti na tarehe 2 Septemba, 2017 kama inavyoonekana kwenye tangazo la kuitwa kwenye usaili.

Mpangilio wa kufanya usaili huo katika Mikoa/kanda kumi umepangwa kwa kuzingatia anuani za waombaji kazi na Jiografia ya Nchi yetu ili kusogeza huduma karibu na wananchi.

Mgawanyo wa Mikoa/kanda hizo ni kama ifuatavyo.

Waombaji kazi wenye anuani za Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara usaili utafanyika Arusha.

Waombaji kazi wenye anuani za Mikoa ya Mbeya, Katavi, Rukwa na Songwe, usaili utafanyika Mbeya

Waombaji kazi wenye anuani za mikoa ya Iringa, Njombe na Ruvuma, usaili utafanyika Iringa

Waombaji kazi wenye anuani za Mikoa ya Mtwara na Lindi usaili utafanyika Mtwara.

Waombaji kazi wenye anuani za Mikoa ya Morogoro na Tanga, usaili utafanyika Morogoro

Waombaji kazi wenye anuani za Mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu, Geita na Kagera, usaili utafanyika Mwanza

Waombaji kazi wenye anuani za Mikoa ya Tabora, Kigoma na Shinyanga usaili utafanyika Tabora

Waombaji kazi wenye anuani za Mikoa ya Dodoma na Singida usaili utafanyika Dodoma

Waombaji kazi wenye anuani za Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani usaili utafanyika Dar es Salaam na

Waombaji kazi wenye anuani za Zanzibar, usaili utafanyika Mjini Unguja.

Aidha kila msailiwa anapaswa kuzingatia kituo alichopangiwa kufanya usaili kama ilivyoainishwa kwenye tangazo la kuitwa kwenye usaili. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.