Placements

Visitors Counter

»Today   14               
»Week   14198               
»Month   80899               
==============
»Total  21671423        

TANGAZO KWA UMMA

June 14, 2017


Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoanza tarehe 16-23 Juni, 2017 imejiandaa kukutana na kuwasiliana na wadau mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu na ufafanuzi wa hoja na maswala mbalimbali  juu ya utekelezaji wa majukumu yake. Sekretarieti ya Ajira tumekuwa tukipokea maswali/maoni/hoja mbalimbali zinazohusu uendeshaji wa mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma.

Katika maadhimisho hayo kwa mwaka huu 2017 Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwakaribisha wadau na wananchi wote kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni, 2017 ambao wangependa kutembelea ofisi za Sekretarieti ya Ajira ili kupata ufafanuzi kuhusiana na majukumu yanayotekelezwa na taasisi yetu kwa kuwa  itakuwa ikitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira zilizopo katika Jengo la Maktaba Kuu ya Taifa ghorofa ya pili  kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 10:30 jioni.

Aidha, kwa wananchi ambao hawatapata fursa ya kututembelea ofisini wanaweza kuwasilisha hoja/ maoni/maswali kwa kupiga simu katika namba zifuatazo na kuongea moja kwa moja na Watendaji wa Sekretarieti ya Ajira ili kupata majibu ama ufafanuzi wa maswali yao kwa kupiga simu 0762-752968, 0784-398259 au 0687- 624975, Pia wanaweza kutuma ujumbe mfupi kupitia anwani zifuatazo; malalamiko@ajira.go.tz, gcu@ajira.co.tz, facebook.com/psrsajira, twitter.com/psrsajira na Instagram psrsajira ambapo yatajibiwa papo hapo.

Imetolewa na;

 Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, 14 Juni, 2017.