Visitors Counter

»Today   224               
»Week   224               
»Month   16776               
==============
»Total  23367162        

Sekretarieti ya Ajira yawaaga Watumishi wanne waliostaafu.

December 12, 2017


Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imewaaga waliokuwa Watumishi wa wanne wa Ofisi hiyo ambao wamestaafu baada ya kumaliza muda wao wa Utumishi Serikalini.

Watumishi walioagwa ni pamoja na Bw. Simion Millanga (Aliyekuwa Mchumi Mkuu) Bibi Godriver Ngwiye (Aliyekuwa Mtunza kumbukumbu mkuu), Bibi Nusura Mohamed (Aliyekuwa Katibu Muhtasi) na Bibi Hawa Komba aliyekuwa Mhudumu wa Ofisi.

Katika hafla ya kuwaaga watumishi hao, Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi aliwashukuru watumishi hao kwa mchango walioutoa wakiwa Sekretarieti ya Ajira na Serikali kwa Ujumla. Aliongeza kuwa watumishi hao ambao baadhi walikuwa miongoni mwa waanzilishi wa Ofisi ya Sekretarieti ya Ajira walisaidia kujenga misingi ya uwajibikaji, uwazi na utekelezaji wa majukumu kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.

“Tunawashukuru sana kwa mchango wenu katika utumishi wa Umma hasa mlipokuwa Sekretarieti ya ajira ambapo miongoni mwenu mlikuwa watumishi wakati Ofisi hii inaanzishwa na kufanya kazi kwa bidii ambapo mchango wenu umesaidia kujenga heshima ya ofisi yetu, ni imani yangu kuwa misingi mliyoijenga itakuwa  chachu ya sisi tunaobaki kuendelea kufanya kazi kwa misingi ya uadilifu, uwazi na kufuata sheria, kanuni na taratibu katika kuwahudumia wadau wetu” aliongeza Daudi.

Kwa upande wake Bi Nusura Mohamedi ambaye alizungumza kwa niaba ya wastaafu wenzake alibainisha kuwa, wanajivunia kuwa sehemu watumishi wa Sekretarieti hiyo hadi kustaafu kwao na kuwaasa watumishi wengine kuendelea kufanya kazi kwa bidii na maarifa zaidi katika kuwahudumia wananchi.

 

Katika Hafla hiyo watumishi hao walitukiwa vyeti na Uongozi wa Sekretarieti ya Ajira kama sehemu ya kumbukumbu kwao na kuenzi historia ya utendaji kazi wao katika Utumishi wa Umma.