PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT

PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT
TANGAZO
Monday, 18 May 2015 16:57

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira anawatangazia waombaji wa Kazi ya LAND OFFICER II walio orodheshwa hapa chini, ambao wamesoma LAND MANAGEMENT AND VALUATION walio takiwa kufanya Usaili wa mchujo tarehe 25/5/2015 wasifike kwenye usaili huo, kwani wao wanatakiwa kufanya usaili tarehe 20/5/2015 kwa Kada ya MTHAMINI. Tafadhali atakaye liona Tangazo hili amwambie na mwenzake.

Read more...
 
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UJAZAJI WA TAARIFA SAHIHI KWENYE MFUMO WA RECRUITMENT PORTAL.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa Umma, Bwana Xavier Daudi, anaendelea kuwasisitiza waombaji kazi kuwa wahakikishe wanaingiza taarifa zao hususan za kitaaluma kwa uhakika na kufuata maelekezo yanayotolewa kwa kila tangazo la kazi husika. Pia Daudi amesisitiza kuwa barua ya maombi ya kazi inapaswa kuambatishwa kwenye sehemu uliyoandikwa other attachments na taarifa zingine ziambatanishwe kwenye kila kipengele kadri zilivyogawanywa kwenye mfumo huo.
Daudi ameongeza kuwa kwa muombaji kazi ambaye atatuma maombi ya kazi kwa kutumia mfumo wa Recruitment Portal bila kujaza taarifa zake kwa ufasaha atambue kuwa maombi yake hayatakubaliwa.
Read more...
 
Taarifa kwa Umma kuhusu Recruitment Portal
Tuesday, 17 March 2015 10:58

Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa umma hivi karibuni ilianzisha majaribio ya kupokea maombi kazi kwa njia ya kielektroniki kwa kutumia ‘Recruitment Portal’ ikiwa ni hatua za majaribio kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa mfumo huu hivi karibuni.

Attachments:
Download this file (Recruitment Portal User Manual.pdf)How to apply[How to apply]2285 Kb
Read more...
 

Contact Address


Maktaba Complex, Second Floor,
Bibi Titi Mohamed Road
Dar es Salaam
P.O Box: 63100
Tel: +255(22) 2153517
Fax: +255(22) 2153518
Email:katibu@ajira.go.tz

Complaints/Malalamiko: malalamiko@ajira.go.tz

Advertised Posts (Nafasi za Kazi)

You are here  : Home