MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO-Business Analyst II & Systems Administrator II-TRA

Posted on September 24, 2017 at 02:30 PM

Kwa wasailiwa waliochaguliwa (SELECTED) kuendelea na usaili wa mahojiano (Oral Interview) wanapaswa kuja na vitambulisho pamoja na vyeti vyao halisi (Original Certificates) Usaili huo utafanyika tarehe 25-09-2017 katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira-Maktaba Kuu ya Taifa , kunzia saa moja kamili asubuhi

 

Read More

MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO KWA WAOMBAJI KAZI NAFASI ZA TRA.

Posted on September 18, 2017 at 05:51 AM

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi waliofanya usaili wa mchujo kwa nafasi mbalimbali za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa matokeo ya usaili huo yamekwishatolewa kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira www.ajira.go.tz

Tarehe ya usaili wa hatua inayofuata kwa kada zenye Usaili wa Vitendo na usaili wa ana kwa ana (Oral Interview) imeainishwa kwa kila kada kwenye matokeo hayo kuanzia tarehe 23 -28 Septemba, 2017.

Read More

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Posted on August 24, 2017 at 11:51 AM

Serikali katika mwaka wa fedha uliomalizika 2016/2017 iliahidi kutoa Ajira serikalini zaidi ya 52,000 kwa Watanzania, ambapo katika siku za hivi karibuni Serikali imekuwa ikitoa vibali vya kuajiriwa watumishi wa kada mbalimbali ikiwemo Waalimu wa Sayansi, Kada za Afya na maeneo mengine kulingana na mahitaji.

Read More

MPANGILIO WA USAILI WA MCHUJO (WRITTEN INTERVIEW) WA KADA ZA TRA UTAKAOFANYIKA KATIKA KANDA 10.

Posted on August 23, 2017 at 08:34 PM

Waombaji kazi waliochaguliwa kwa ajili ya usaili wa Mchujo wa nafasi mbalimbali za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zilizotangazwa hivi karibuni wanataarifiwa kuwa usaili wa hatua ya mchujo utafanyika katika Mikoa/kanda 10 kuanzia tarehe 30, 31 Agosti na tarehe 2 Septemba, 2017 kama inavyoonekana kwenye tangazo la kuitwa kwenye usaili.

Read More

ANGALIZO KWA WAOMBAJI WA NAFASI ZA KAZI

Posted on July 4, 2017 at 11:57 AM

Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwasisitizia waombaji wote kusoma kwa makini tangazo la nafasi za kazi na kuzingatia sifa za msingi na maelekezo yaliyotolewa kabla ya kutuma maombi ikiwemo kuthibitisha (Certify) Nyaraka (Vyeti) pamoja na kuweka sahihi (Signature) katika barua ya maombi ya kazi ambayo imeainisha nafasi inayoombwa.

Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya kielektroniki katika “recruitment portal” http://portal.ajira.go.tz ya Sekretarieti ya Ajira.

Read More